Deuteronomy 26

Malimbuko Na Zaka

1Mtakapokuwa mmeingia nchi ile ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake, 2 achukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali ambapo Bwana Mwenyezi Mungu wako atapachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake 3na umwambie kuhani atakayekuwepo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayo Bwana aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.” 4Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu ya Bwana Mwenyezi Mungu wako. 5 bKisha utatangaza mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. 6 cLakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. 7 dKisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. 8 eKwa hiyo Bwana akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu. 9 fAkatuleta mahali hapa akatupa nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali; 10 gnami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee Bwana, umenipa.” Weka kapu mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wako na usujudu mbele zake. 11 h iKisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.

12 jWakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba. 13 kKisha umwambie Bwana Mwenyezi Mungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo. 14 lSijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yoyote kwa wafu. Nimemtii Bwana Mwenyezi Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru. 15 mAngalia chini kutoka mbinguni, maskani yako matakatifu, uwabariki watu wako Israeli pamoja na nchi uliyotupa kama ulivyoahidi kwa kiapo kwa baba zetu, nchi inayotiririka maziwa na asali.”

Fuata Maagizo Ya Bwana

16 n Bwana Mwenyezi Mungu wako anakuagiza leo kufuata amri hizi na sheria; zishike kwa bidii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. 17 oUmetangaza leo kwamba Bwana ndiye Mungu wako na kwamba utafuata njia zake, kwamba utayashika maagizo yake, amri zake na sheria zake nawe utamtii. 18 pNaye Bwana ametangaza leo kwamba ninyi ni taifa lake, hazina yake ya thamani kama alivyoahidi, ili kwamba mpate kuyashika maagizo yake yote. 19 qAmetangaza kwamba atawaweka juu kuliko mataifa mengine aliyoyafanya katika sifa, kuwa fahari na heshima, na kwamba mtakuwa taifa takatifu kwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu, kama alivyoahidi.
Copyright information for SwhKC